top of page
  • Kevin Lumenello

Balaa wa Lewiston

10/27/23


Merikani ni kawaida kuskia habari za ukaukaji. Kuskia kuhusu vifo vya watu ambao hawajafanya chochote kustahili shambulio. Vifo kama hivi vimeongeza maradufu ndani ya miaka za hivi karabuni. Niliwaza majimbo yenye hatari zaidi Florida, Texas, California lakini sio jimbo langu wa Maine.Hapa Maine ndani ya mwaka Idadi ya watu ambao wamekufa na risasi ni kama ishirina. Juzi tulehesabu zaidi ya kumi na tano


Mwezi uliyopita Mungu alinipenafasi ya kununua nyumba. Niliamua kuhamia Lewiston, mji ambapo kuna watu wa kazi, mbali kidogo na utalii ya Maine. Mji ambapo famalia, wahamiaji mbalimbali, na pia watu sio wa utajiri sana wanaishi pamoja kwa usalama. Sahemu napopenda sana.


Lewiston inajulikana na jina baya kama watu wa hapa ni duni lakini sio kweli. Labdha kwa sababu hatuna bahari hatuna utalii. Hasa kwa kichekesho tunajulikana kama ‘Dirty L’ ( Uchafu L)


Alafu habri ya vifo kubwa sana mno inafika. Inkaonyesha picha gani ? Mji pabaya pamekuwa pabaya zaidi kabisa. Lakini sio mkosa kwa sababu wa mji wala watu wake. Balaa kama hii inaweza kutokea popote tu.


Shambulio kama hill linasababisha habari kubwa sana. Nilipigwa bambuazi kumuona mwanahabari Lester Holt yupo kwa mji wangu moja kwa moja kutoka Israel.Walewiston Tumeagizwa tubaki ndani kwa ajili ya usalama. Nilitoka tu kuona mtaa. Magari yameadimika sana kasoro za polisi. Hata Helicopta zimezunguka kabisa sauti yake imeenea kila sehemu.


Maofisini, Madukani, Na shuguli nyingi zimefungwa. Polepole mambo yatarudi kama kawaida lakini mabadirisho wa mji yatakuwa mengi. Hatutaweza kusahau daima. Mungu wasaidie wale wathirika kabisa. Tusaidie jamii yetu.


Comments


bottom of page