top of page

 

Karibuni Sana

 

Mambo vipi ndugu zangu? Tangu nilikuwa mtoto mdogo na miaka kumi na nne nilipenda sana kupiga chuma. Nimefundishwa vizuri sana sasa nataka nasambaa elimu yanngu na nyinyi. Katika video zangu natawafundisha jinsi ya kuongeza misuli na ya kupunguza kitambii. Video nyingi wa Ulaya haizifanya kazi kwa sababu hawizingatii utamaduni wala maisha zetu. 

 

Lugha yetu- Elimu yetu

 

Twendeni Tufanye Kazi Pamoja!

 

Hello everyone, this page is dedicated to my fitness content. I’ve noticed how lacking the internet is with information in the Swahili language. This is my way to contribute to the beautiful language. Even if you don’t speak Swahili feel free to watch my videos and learn something about the exercise culture of East Africa !

Jinsi Ya Kuongeza Nyama Mwilini

 

 

 

Asalam alikum. Bwana Yesu Asifiwe. mambo vip..? Karibuni sana mimi ni kevomswahili na hii ni Elimu fitness. Leo tunazungumza kuhusu jinsi ya kuongeza nyama mwilini wengine wana sema Kuongeza misuli , sio kitu rahisi sanaaa ila ukizingatia haya mambo matano! Yafwatayo hakika utaweza! 

 

Karibu sana ndani ya kevomswahili  nahii ni  Elimu fitness na leo tupo mitaa ya uswahilini natafuta gym kwajiri ya kufanya mazoezi katika siku yangu ya leo.

Twende pamoja tukafanye mazoezi mtaani.


 

Kama ifuatavyo, MAZOEZI , KUTO KUTUMIA VILEVI, CHAKULA, KUPATA USINGIZI WA KUTOSHA, NIZAMU.

 

(v.o)

5 Mazoezi

Mazoezi kweli yanatengeneza njia nzuri ya kuongeza mwili. Unahitaji kufanya mazoezi  yanajulikana kwa Kiingereza “Resistance training” mazoezi ambayo unatumia misuli, Mazoezi kama pushups na situps, lakini muhimu sana kupiga chuma. Unaweza fanya mazoezi bila vifaa vyovyote kama - squats, Pushups, Lunges, na mazoezi mengi ya abs, hata unaweza kuvaa begi lenye uzito kwa kuongeza nguvu yako. Hizo ni nzuri lakini kwenda gym ni nzuri zaidi. Kwa gym unaweza kufanya mazoezi mazuri kama bench press, sholder press, na bicep curls. Kwa gym unaweza fanya aina nyingi sana ya mazoezi na ku-train mwili wako mzima. Wakati unafanya mazoezi kesho yake lazima nyama ziume, inamanaa kwamba ulifanya mazoezi magumu  sana. usijali utapona lakini hadi utakapozoea mazoezi. Ni nzuri kama unapendela misuli mikubwa katkika mwili wako kama vile miguu, kifua, mabega, na mgongo , Pia inabidii unafanya mazoezi yako menye ya nguvu sana mpaka uchoke kabisa. Unahitahi kupata 100% ya maumivu  wakati unafanya mazoezi.  Nibora kufanya mazoezi kwa bidii mara 3 kwa wiki kuliko kufanya mazoezi mara 7 kwa wiki kivivu. Inategemea kwa kiwango chako cha  uzoefu wa mazoezi lakini nakushauri siku tatu mpaka siku sita kwa wiki inatosha kuongeza mwili wako.


 

4.kuto kutumia vilevi, 

Kama kijana nakushauri vilevi kama pombe vina madhara mengi katika maisha hasa katika maisha ya mazoezi. Pombe ina zohofisha sana mwili kama unakunywa pombe katika maisha ya mazoezi unaupa mwili  hang over itakayo kufanya ushindwe kwenda  mazoezi kesho yake. Kulewa pia inatengeneza madhara ya kukosa usingizi, kula vibaya, kukosa nidhamu, na kupata matatizo tofautitofauti.

nakuambie kweli moja kwa moja ni ngumu sana kuongeza nyama kama ukinywa pombe sana. Kunywa Mara moja kwa mwezi sio mbaya, mara moja kwa wiki utapoteza faida nyingi sana. 

 

3. Chakula

Chakula na maji pamoja ni uhai, kwa kiingereza tunasema “You are what you eat” inamanaa wewe ni unachokula, ukila vizuri unakuwa na afya nzuri, napia ukila vibaya mwili utadhorota . Hakikisha unakula vyakula vya kukupa nguvu kama ubwabwa mahage, ugali, mkate, tambi pamoja na mboga mboga za majani na matunda. Kitu muhimu sana pia kula vyakula vya proteni. Kuna faida nyingi sana ya kula protini ya kutosha lakini sana Kuongeza nyama mwilini proteni inapatikana katika vyakula kama nyama, maziwa, mayai, njugu, korosho  na kwa bei rahisi sana na chakula ninacho penda sana ni ubwabwa  maharage. Jaribu kula proteni kila wakati unapokula hata kama ni kidogo. Mara kwa mara zingatia kula udambu udambum, kama vitumbua, sambusa, kachori, bagia, na mandazi. Kuchangamsha mwili wako.

 

2 Kulala vizuri

Kupata muda wa kutosha kulala ni muhimu sana kwa binadamu  hasa kwa wafanya mazoezi . Kama unafanya mazoezi kwa bidii na unakula vizuri unahitaji kuupa mwili muda wa kutosha kupumzika. Ukilala mwili unajenga misuli na kupata nguvu mpya. Hata kama utakosa usingizi  kwa kuchoka sana na kushindwa  ku-preform gym au kukosa kabisa  gym. Najua maisha yanaenda kasi sana yana kufanya kuwa busy sana na heka heka nyingi lakini kama unaweza nakushauri upate kati ya masaa saba mpaka masaa tisa sio mbaya kulala  kwa siku.


 

1 Nidhamu

 

Hakuna kitu kizuri utakipata rahisi maishani. Kwa hiyo unahitaji kuwa na Nidhamu sio mazoezini tu, wakati wote. Kama unakosa chakula na usingizi na bado unafanya mazoezi huwezi kupata faida nzuri mwilini mwako. Huwezi kuacha kujali kuhusu afya yako au Kushindwa kuheshimu ratiba yako. Ni muhimu sana kufuata nia yako kila siku. jenga ratiba yako ya mazoezi vivuri pamoja na vitu vingine vya muhimu kama vile  familia, kazi, na dini lakini usisahau kujali kuhusu Afya yako. Kupata faida haraka sio rahisi Ila ukiwa na nidhamu nzuri ya kuheshimu kanuni za mazoezi ni rahisi sana kujenga mwili wako, Inabidii unaangalia faida kwa mwezi sio kwa wiki. Ukiona nyama azikui fikiria kuhusu unavyofanya alafu fanya marekebesho na jaribu tena na tena kupitia kanuni hizi tano.

Body Building Routine - Nairobi Kenya

Cheap Protein in Mombasa Kenya

bottom of page